Habari
HATUTAMVUMILIA MWAJIRI YEYOTE ATAKAYESHINDWA KUSIMAMIA HAKI NA STAHIKI ZA WATUMISHI WA UMMA-Mhe. Jenista

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza hoja za watumishi wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro kilicholenga kuhimiza uwajibikaji. Walioketi wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wake Mhe. Ridhiwani Kikwete, wa pili ni Naibu Waziri wa Afya, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Siha, Mhe. Godwin Mollel na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Siha, Mhe. Dkt. Christopher Timbuka.