Maswali na Majibu

Ufafanuzi kuhusu gharama za uhamisho kutoka kituo kimoja cha kazi kwenda kituo kingine

Kwa mujibu wa Kanuni J.2, L.5 na L.13 ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma za mwaka 2009 mtumishi anayehamishwa anastahili ya kulipwa posho ya kujikimu kwa siku kumi na nne (14) kwa ajili yake, mwenzi, na hadi watoto wanne; Posho ya usumbufu na Mizigo yake tani tatu (3). Hata hivyo Kwa mujibu wa Kanuni L.8 ya kanuni hizo kwa watumishi wanaojiombea uhamisho mwajiri ana hiari ya kumlipa au kutomlipa kutokana na mazingira ya uhamisho wake pamoja na upatikanaji wa fedha.