English | Swahili

Frequently Asked Questions - All FAQs

Please select your question category

View all frequently asked questions
View featured frequently asked questions
No faqs found in this category

Mtumishi wa umma aliyepata ajali, kuumia au kufariki akiwa kazini anatakiwa atoe taarifa kwa mwajiri wake kisha mwajiri afuate taratibu zifuatazo:-
•Mwajiri anapaswa kuwasilisha taarifa ya awali kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma huku akiendelea kuunda kamati ya uchunguzi wa ajali Kanuni 111(1) na 111(2) yahusika.
•Baada ya kamati ya uchunguzi kukamilisha taarifa, mwajiri anapaswa kuwasilisha taarifa hiyo kwa Katibu Mkuu (Utumishi) ikiwa na mapendekezo yake mintaarafu Kanuni 111(5).
•Katibu Mkuu – Utumishi atawasilisha mapendekezo yote pamoja na ushauri wake kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kuamua kiwango cha malipo ya fidia kwa mtumishi aliyepata ajali akiwa kazini hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 112. 

  • Ili kuongeza uwajibikaji, kila Taasisi ya Umma inatakiwa iwe na Mkataba wa Huduma kwa Mteja.Mkataba wa Huduma kwa Mteja unawapa fursa wateja kuelewa ubora wa huduma zinazotolewa na taasisi za umma. Kimsingi,na kwa kuwa kila Wizara kwa sasa tayari ina mfumo wa utendaji wa kimenejimenti ambayo mojawapo ya mahitaji ni kuwa na mkataba wa huduma kwa mteja
  • Suala la ajira mpya linategemea na kuwepo kwa mahitaji halisi ya kuwa na mtumishi mpya na inatakiwa kuingizwa kwenye bajeti (Ikama).Nafasi ambazo ziko wazi kabla ya kujazwa lazima fedha itengwe (Bajeti) kwa ajili ya watumishi watakaoajiriwa.Jukumu hili ni la mwajiri mwenyewe ambaye anawajibu wa kuangalia maeneo yanayohitaji rasilimali watu.Hata hivyo,kama zilivyo nafasi za ajira mbadala,kwa nafasi mpya pia ni lazima zipatiwe vibali vya ajira mbadala,kwa nafasi mpya pia ni lazima zipatiwe vibali vya ajira pamoja na kufuatwa kwa taratibu za ajira kwa mujibu wa Sera ya Menejimenti na Ajira ya mwaka 1999 na Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8 ya mwaka 2002 pamoja na marekebisho yake Na.17 ya mwaka 2007.

Pia katika Sekta ya Afya ni vigumu kutumia mfumo wa OPRAS.

·       Utaratibu wa Upimaji Utendaji Kazi kwa Wazi (OPRAS) unaendana na mwaka wa fedha wa serikali.Hata hivyo hauna tatizo kwani kinachoangaliwa ni malengo yaliyowekwa katika kipindi cha miezi kumi na mbili (12). Hivyo kila Mtumishi wa Umma katika sekta zote zikiwemo Elimu na Afya wanaweza kutekeleza mfumo huo wa OPRAS.

 

Iwapo mtumishi wa umma ambaye hajaridhika na adhabu aliyopewa iliyotokana na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa utaratibu ulio rasmi na ule usio rasmi anaweza kukata rufaa kama ilivyoonyeshwa katika Jedwali lililotangulia.

Katika Utumishi wa Umma zipo aina mbili za ushughulikiwaji wa makosa ya kinidhamu. Aina hizo ni:-
(i)Makosa yanayoshughulikiwa kwa utaratibu rasmi (formal proccedings)-Kanuni 42(1) Kanuni za Utumishi wa Umma,2003
(ii)Makosa yanayoshughulikiwa kwa utaratibu usio rasmi(summary proceedings-Kanuni 43(1), Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003
•Makosa yanayofaa kushughulikiwa kwa utaratibu ulio rasmi pamoja na adhabu zimeorodheshwa katika Jedwali la Kwanza, Sehemu ‘A’ ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003
•Makosa yanayofaa kushughulikiwa kwa utaratibu usio rasmi pamoja na adhabu zimeorodheshwa katika Jedwali la Kwanza, Sehemu B, Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003

·       Serikali haina ubaguzi wa Watumishi wake ila inawajali wote kwa misingi ya Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyopo.Suala la utekelezaji wa OPRAS ni suala la watumishi wote wa umma.Utaratibu wa OPRAS umeingizwa rasmi kwenye Sheria ili kutilia mkazo uwajibikaji na ufanisi wa utekelezaji wake. OPRAS inapaswa kuandaliwa kulingana na rasilimali zilizopo hata kama ni kidogo na kila Mtumishi wa Umma anapaswa kutekeleza OPRAS.

Mamlaka ya kulipa fidia itatoa taarifa ya kiwango cha fidia kwa mwajiri na endapo fidia husika imeridhiwa, mwajiri wa mtumishi atapaswa kuandaa malipo hayo na pale mwajiri anaposhindwa kulipa fidia husika anaweza kuwasilisha maombi hayo Hazina.

Mamlaka ya kulipa fidia itatoa taarifa ya kiwango cha fidia kwa mwajiri na endapo fidia husika imeridhiwa, mwajiri wa mtumishi atapaswa kuandaa malipo hayo na pale mwajiri anaposhindwa kulipa fidia husika anaweza kuwasilisha maombi hayo Hazina.

·       Mwajiri ambaye hataridhika na uamuzi uliotolewa na mamlaka ya rufaa anaweza kukata rufaa kwa mamlaka ya juu ya rufaa inayostahiki.

Sio kweli kuwa kwenye mfumo wa Utumishi watu wenye elimu ndogo ndio wanaopangwa vijijini.Utaratibu uliopo ni wa kuhakikisha kuwa watumishi wanapangwa sehemu mbalimbali za nchi kulingana na mahitaji.

Ili mtumishi wa umma aweze kulipwa mshahara binafsi inatakiwa apate kibali cha mshahara binafsi kinachotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mintaarafu   mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 Kifungu Na. 8 (3) (e) kikisomwa kwa pamoja na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma Toleo la Mwaka 2009 Kanuni E.1.

Taratibu zinazotumika kumpandisha cheo mtumishi wa umma zimeainishwa katika Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ya mwaka 2008 ikisomwa kwa pamoja na Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003 kama ifuatavyo:-
i)    Kuwepo kwa nafasi iliyotengewa fedha katika mwaka wa fedha husika,
ii)    Muundo wa utumishi (scheme of service) wa kada husika,
iii)    Utendaji mzuri wa kazi,
iv)    Orodha ya ukubwa kazini (seniority list),
v)    Maendeleo ya kitaaluma (career development),
vi)    Urithishanaji wa madaraka (succession plan).    

Vigezo vilivyotumika kupanga mishahara ya sasa ni ripoti ya zoezi la tathmini ya kazi (Jo Evaluation exercise) lililofanyika mwaka 1998.    

Mtumishi wa umma anatakiwa awe na nakala ya vitu vifuatavyo ili aweze kulipwa pensheni;-
i.Barua ya kustaafu.
ii.Barua ya kuajiriwa kwa mara ya kwanza Serikalini.
iii.Barua ya kuajiriwa katika masharti ya kudumu na pensheni
iv.Barua ya kuthibitishwa kazini.
v.Barua ya kupandishwa vyeo mbalimbali wakati wote wa Utumishi Serikalini.
vi.Fomu ya ‘retiring award’.

Mtumishi wa umma anapaswa kuwa na vitu vifuatavyo katika kushughulikia masuala ya mirathi:-

i.Cheti halisi (original) cha kifo kilichotolewa na Ofisi ya Msajili wa Vizazi na Vifo.
ii.Hati halisi (original) ya msimamizi wa mirathi iliyobandikwa picha ya msimamizi.
iii.Nakala ya cheti cha ndoa.
iv.Kiapo cha mjane kinachotolewa na Mahakama na chenye picha ya mjane.
v.Kiapo cha kutunza watoto chenye picha ya anayetunza watoto kinachotolewa na Mahakama.
vi.Nakala ya Vyeti vya kuzaliwa watoto wa marehemu wenye umri usiozidi miaka 21.
vii.Picha mbili (passport size) za msimamizi wa mirathi,watoto wa  marehemu na mjane zilizogongwa muhuri wa Mahakama.

Makosa yanayoshughulikiwa kwa utaratibu ulio rasmi (formal proccedings) yana hatua zifuatazo:-
(i)Mamlaka ya nidhamu inapaswa kufanya uchunguzi wa awali ili kujiridhisha kama iko haja ya kuchukua hatua za kinidhamu kabla ya kuanza mchakato wowote wa kinidhamu (Kanuni 36, Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003)
(ii)Iwapo mamlaka ya nidhamu itajiridhisha kuwa kosa limefanyika, basi itampa mtumishi Hati ya Mashtaka na Notisi kumweleza kosa/makosa anayotuhumiwa kufanya na anayolazimika kuyajibu kupitia utetezi wake(Kanuni 44(1), Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003)
(iii)Mamlaka ya nidhamu inaweza kumsimamisha kazi mtumishi ambaye suala lake la kinidhamu linashughulikiwa ili kuwezesha ushughulikiwaji wa suala hilo kufanyika (Kanuni 38 na 39 za Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003)
(iv)Ikiwa utetezi au majibu ya mtumishi anayetuhumiwa hautoshelezi kumtoa hatiani, mamlaka ya nidhamu itaunda Kamati ya Uchunguzi (Kanuni 45(1) Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003) kwa ajili ya kuchunguza suala hilo ikiwa ni pamoja na kumhoji mtumishi husika, mashahidi n.k.
(iv)Kama majibu ya  mtumishi baada ya kupokea Hati ya Mashtaka yanaonyesha kukubali kutenda kosa, mamlaka ya nidhamu haitalazimika kuunda Kamati ya Uchunguzi na itaendelea kutoa adhabu stahiki (Kanuni 45(3) Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003).

 

Usimamizi wa masuala ya nidhamu katika Utumishi wa Umma uko chini ya mamlaka mbalimbali za nidhamu. Mamlaka za nidhamu, watumishi wanaohusika na ngazi za rufaa zinafafanuliwa kama inavyoonekana katika Jedwali lifuatalo:- 

Aina ya watumishi

Mamlaka ya Ajira

Mamlaka ya Nidhamu

Rufaa ya Kwanza

Muda wa Kukata Rufaa

Rufaa ya Pili

Muda wa Kukata Rufaa

Watumishi ambao huteuliwa na Rais. 

Rais (Kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298

Katibu Mkuu Kiongozi (Kifungu cha 4(3)(d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 na  Kanuni ya 35(2)(a) ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003

Rais (Kifungu cha 25(1)(a) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298

45 (Kanuni ya 61 ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003)

-

-

Watumishi ambao mamlaka yao ya ajira si Rais na masharti yao ya kazi ni ya Kudumu na Malipo ya Uzeeni.

Katibu Mkuu, Watendaji Wakuu wa Wakala, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi Halmashauri za Majiji, Miji, Manispaa na Wilaya (Kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298)  

Waziri mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Katibu Mkuu, Mtendaji Mkuu wa Wakala, Katibu Tawala wa Mkoa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa, Mji na Wilaya (Kifungu cha 6(3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298

Tume ya Utumishi wa Umma (Kifungu cha 25(1)(b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298

45(Kanuni ya 61 ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003)

Rais (Kifungu cha 25(1)(c) ya Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298)

45(Kanuni ya 6(1) ya Kanuni ya Utumishi wa Umma, 2003)

Watumishi wa Huduma za Kawaida ( Operational Service)

Katibu Mkuu, Watendaji Wakuu wa Wakala, Makatibu Tawala wa Mkoa, Wakurugenzi Halmashauri za Majiji, Miji, Manispaa na Wilaya

Wakuu wa Idara/Vitengo (Kifungu cha 6(3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298)

Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (Kanuni ya 60(4) ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003)

45(Kanuni ya 6(1) ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003)

Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi (Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini, 6/2004)

 

 

·        Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma (ina utaratibu wa kuwahimiza waajiri wote kama:Wizara,Idara Zinazojitegemea,Wakala na Sekretarieti za Mikoa kutunza kumbukumbu za watumishi ambao wako masomoni na watakaokuwa masomoni na kuwasilisha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kila mwaka wa fedha kupitia miongozo na nyaraka mbalimbali ikijumuisha mipango na mahitaji ya mafunzo ya kila taasisi.Aidha, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ina utaratibu wa kuhifadhi kumbukumbu kwa watumishi ambao wako masomoni nje ya nchi.Utaratibu huu unaendelea kuboreshwa kwa kuwatambua watumishi ambao hawarejei nyumbani mara baada ya kumaliza masomo yao kwa kushirikiana na waajiri.

·       Inawezekana kuwapo kwa tofauti ya fomu za Upimaji Utendaji Kazi wa Wazi (OPRAS) kwa kada.Kwa mfano tayari Walimu wanayo fomu ya OPRAS inayoendana na matakwa ya kada yao.

Kwa mujibu wa Waraka wa Utumishi Na.2 wa mwaka 2014 kuhusu kudhibiti Virusi Vya UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa mahali pa Kazi katika Utumishi wa Umma, Mamlaka za Ajira zina wajibu wa kuwahudumia watumishi waliojitokeza kuwa wanaishi na VVU na UKIMWI kwa kuwapatia fedha kiasi kisichopongua Shs. 50,000/= na kisichozidi Sh. 100,000/= kwa mwezi. Aidha, watumishi wanatakiwa kuwezeshwa na kupatiwa mafunzo na huduma ya ushauri nasaha mara kwa mara.  

Walimu walioajiriwa kwa Mkataba (Leseni), wanatakiwa kujiendeleza katika fani ya Ualimu (Elimu) ndani ya kipindi cha miaka mitano kuanzia 2007 hadi 2012. Hivyo kama amejiendelea katika fani ambayo siyo ya Ualimu anatakiwa kutafuta ajira upya Serikalini kwa kutumia fani aliyosomea na sio kubadilishwa kazi.

Kwa mujibu wa Kanuni H.5 ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma za mwaka 2009; Nauli ya Likizo hulipwa mara moja katika mzunguko wa miaka miwili. Nauli hiyo hulipwa kwa mtumishi, mwenzi na wategemezi wasiozidi wanne kwa kuzingatia viwango vya nauli vinavyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA).

Kwa mujibu wa Kanuni J.2, L.5 na L.13 ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma za mwaka 2009 mtumishi anayehamishwa anastahili ya kulipwa posho ya kujikimu kwa siku kumi na nne (14) kwa ajili yake, mwenzi, na hadi watoto wanne; Posho ya usumbufu na Mizigo yake tani tatu (3). Hata hivyo Kwa mujibu wa Kanuni L.8 ya kanuni hizo kwa watumishi wanaojiombea uhamisho mwajiri ana hiari ya kumlipa au kutomlipa kutokana na mazingira ya uhamisho wake pamoja na upatikanaji wa fedha. 

 

Kwa mujibu wa Maelekezo ya Katibu Mkuu (Utumishi) katika barua yenye Kumb.Na.CAC.45/257/01/A/83 ya tarehe 9/9/2013 mtumishi anastahili kupandishwa cheo baada ya kutumikia cheo cha awali kwa kipindi cha angalau miaka mitatu (3) kwa kuzingatia TANGE (Seniority list) iliyopo, Sifa za Kimuundo, Kuwepo kwa nafasi iliyoidhinishwa katika Ikama na kuwepo kwa fedha za kugharamia upandishwaji vyeo kwenye bajeti. 

Kwa mujibu wa Kanuni G.7 ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma  za mwaka 2009 ili mtumishi aweze kugharimiwa mafunzo na Serikali yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:-

  • Kuwepo katika Mpango wa Mafunzo ;
  • Kuwepo  bajeti ;
  • Kuwepo kwa ruhusa ya kuhudhuria mafunzo

Kwa mujibu wa Kanuni K.17 ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma za Mwaka 2009, Mtumishi wa Umma aliyepewa Rufaa ili kumwezesha kutibiwa Nje ya kituo chake cha kazi anastahili kulipwa Posho ya Kujikimu.

 

FAQs - All FAQs
No faqs match your search criteria

Quick Links

1611074
TodayToday2578
YesterdayYesterday2733
This_WeekThis_Week3209
This_MonthThis_Month57629
All_DaysAll_Days1611074

Location Map

Quick Contacts

Phone:+255 (026) 2963630
Fax:+255 (026) 2963629
Email :ps@utumishi.go.tz
Website:http://www.utumishi.go.tz

Site Poll

How do you rate our services?