Baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu wakimsilikiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mafunzo maalum kuhusu utekelezaji sahihi wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo katika uendeshaji wa Utumishi wa Umma kwa Watendaji hao, mjini Morogoro.