More Links

Webmail
PSP
FAQ

Agencies

TPSC
TGDLC
PO-PSM Library PDF Print E-mail

UTANGULIZI:

 Maktaba ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ina jukumu la kuendeleza watumishi wa Umma, ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na uwezo wa hali ya juu kama ilivyofafanuliwa katika Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ya Mwaka 1998.  Maktaba hii inahudumia watumishi wote wa umma, watafiti na wananchi.  Maktaba hii inazo sheria, vitabu, kanuni za utumishi, ripoti na machapisho mbalimbali.  Watumiaji wa huduma hii inakaribia watu 80 kwa siku.  Aidha sehemu hii inahariri Gazeti la Serikali. Katika kuhakikisha inatoa huduma bora na kwa ufanisi, maktaba imeanzisha mfumo wa matumizi ya kompyuta katika uazimishaji wa vitabu ambao utatumiwa na watumishi wote kutoka katika wizara, idara zinazojitegemea zikiwemo wakala za serikali pamoja na taasisi za umma. 

 HIFADHI ZA VITABU NA NYARAKA 

Maktaba inavyo vitabu na machapisho yafuatayo:-

  •  Magazeti ya Serikali (Official Gazettes) kuanzia 1957 hadi 2006;
  • Sheria zote za Tanzania;
  • Taarifa mbalimbali zitolewazo na Serikali kupitia katika Gazeti la Serikali (Government Notice) pamoja na sheria ndogo za Halmashauri;
  •  Ripoti za Wizara na za Tume mbalimbali;
  • Vitabu mbalimbali kwa ajili ya kuwaendeleza watumishi katika kada zao;
  • Taarifa za Bunge (Hansard);
  • Kanuni za Utumishi wa Umma;
  • Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Tanzania Government Directory;
  • Nyaraka za Maendeleo ya Utumishi (Establishment Circulars);
  • Nyaraka za Utumishi (Staff Circulars);
  • Machapisho yanayohusu Programu ya Kuboresha Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma;
  • Miongozo na Vitabu vya Maadili ya Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma;
  • Majarida mbalimbali;
  •  Magazeti ya kila siku.
  HUDUMA ZA MAKTABA 
  • Upatikanaji wa sera, kanuni, miongozo kwa ajili ya marejeo au kuazimwa au kuchukua kabisa;
  • Usambazaji wa Nyaraka, Machapisho, Ripoti kwenye Wizara, Mikoa, Halmashauri, Watafiti, Vyuo, Wananchi kwa ujumla;
  • Utoaji wa nakala kwa ajili ya marejeo kwa watumishi wa umma wanaohitaji nyaraka zilizopo;
  • Upokeaji wa matangazo na uhariri wa Gazeti la Serikali;
  • Kusimamia uchapishaji wa nyaraka mbalimbali zinazotolewa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma;
  • Upatikanaji wa vitabu mbalimbali kwa ajili ya kuwaendeleza watumishi katika kada zao;
  • Utunzaji kwa ajili ya marejeo magazeti ya Tanzania ya kila siku kuanzia mwaka 1985;
  • Utunzaji kwa ajili ya marejeo magazeti ya serikali, sheria na taarifa mbalimbali zitolewazo (Government Notice) na sheria ndogo za Halmashauri.
Last Updated ( Wednesday, 03 October 2007 )