Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria iliyolenga kukagua utekelezaji wa mradi wa soko, vyoo na vizimba katika Kijiji cha Lituta, Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Songea tarehe 14.03.2024.