UZINDUZI WA KIPINDI CHA PILI CHA AWAMU YA TATU YA TASAF

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika akitoa maelezo ya awali kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuzindua Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango huo jijini Dar es Salaam leo.