Mkuchika awapongeza watumishi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma kwa kutoa msaada kwa watoto yatima

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akikabidhi msaada wa fedha taslimu na mahitaji kwa mlezi wa kituo cha Swako cha kulea watoto yatima, Bi. Regina Chinguku kilichopo Songea mkoani Ruvuma kwa niaba ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma waliochanga ili kukisaidia kituo hicho.