Mhe.Mkuchika apongeza wanufaika wa TASAF wa kijiji cha Mkwanyule wilayani Kilwa

Mmoja wa wanufaika wa TASAF mkazi wa kijiji cha Mkwanyule Bi. Mwanahamisi Ally Ukwenda akishuhudia namna alivyonufaika na TASAF wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na wanufaika wa TASAF uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani Kilwa. Kushoto kwake ni mnufaika mwenzie Bi. Atili Masoud Swalehe.