Mhe. Mkuchika akutana na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bw. Mohamed Hamad baada ya kikao na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kilichofanyika ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma leo. Kikao hicho kilikuwa na lengo la kujadiliana namna ya kufanya kazi kwa ushirikiano katika masuala ya utawala bora.