Dkt. Mwanjelwa ashangazwa na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kutoa kiwanja kwa wajasiriamali

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimsikiliza Mwenyekiti wa kikundi cha utengenezaji wa milango na madirisha ya chuma, Bw. Abdallah Chunga alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua vikundi vya wajasiriamali waliorasimishwa katika Manispaa ya Morogoro.