Watunza Kumbukumbu na Maafisa Rasilimaliwatu watakiwa kuzingatia uadilifu katika utunzaji kumbukumbu

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akiwa katika kikao kazi cha siku tatu cha Watunza Kumbukumbu na Maafisa Rasilimaliwatu Serikalini chenye lengo la kujadili masuala ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo jijini Dodoma. Wa kwanza kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi