Watumishi 44,800 wa kada ya afya kuajiriwa nchini kwa mwaka wa fedha 2019/20

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Silafu Jumbe Maufi  Bungeni leo jijini Dodoma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililohusu  mpango wa Serikali kuajiri watumishi wa kada ya afya ili kuboresha huduma za afya nchini.