TANZANIA BILA RUSHWA INAWEZEKANA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst.), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizindua Mkakati wa Kitaifa wa Kushirikisha Vijana wa Skauti katika mapambano dhidi ya rushwa nchini katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni Rais Mstaafu na Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania, Mhe. Ali Hassan Mwinyi (kulia), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Rais wa Chama cha Skauti Tanzania, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb) (wa pili kutoka kushoto) na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Justine Mahiga (MB) (kushoto).