Rais Magufuli kuzindua Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst)Mhe. George Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari alipokuwa akizungumza nao kuhusu uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) utakaofanyika siku ya Jumatatu tarehe 17 Februari, 2020 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere , Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu IKULU na Mwenyekiti wa Bodi ya TASAF Dkt. Moses Kusiluka na kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga.