Maswali na Majibu

Watumishi walioajiriwa kwa tiketi ya leseni na kujiendeleza nje ya mfumo wa elimu

Walimu walioajiriwa kwa Mkataba (Leseni), wanatakiwa kujiendeleza katika fani ya Ualimu (Elimu) ndani ya kipindi cha miaka mitano kuanzia 2007 hadi 2012. Hivyo kama amejiendelea katika fani ambayo siyo ya Ualimu anatakiwa kutafuta ajira upya Serikalini kwa kutumia fani aliyosomea na sio kubadilishwa kazi.