Maswali na Majibu

Utaratibu wa kulipwa nauli ya likizo pamoja na gharama halisi za likizo

Kwa mujibu wa Kanuni H.5 ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma za mwaka 2009; Nauli ya Likizo hulipwa mara moja katika mzunguko wa miaka miwili. Nauli hiyo hulipwa kwa mtumishi, mwenzi na wategemezi wasiozidi wanne kwa kuzingatia viwango vya nauli vinavyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA).